browser icon
You are using an insecure version of your web browser. Please update your browser!
Using an outdated browser makes your computer unsafe. For a safer, faster, more enjoyable user experience, please update your browser today or try a newer browser.

Watoto Kenya Onlus

logo_e_sito_2_lines_AB

Contact Person: Francesco Moschini; Telephone Number: +39 3491829119;
E-mail: eventi@watotokenya.org;
Website: www.watotokenya.org

Xlestrade ilikutana na Lara Bertoncello na Frarncesco Moschini, wafanyakazi wakujitolea na wasemaji wa Watoto Kenya Onlus kule Padova.
10410951_318999504969975_6133421015012683200_nWatoto Kenya Onlus ilizaliwa mwaka wa 2004 na kikundi cha marafiki kutoka Roma. Wakifuata ushauri wa Sabrina Sabbatini na Italo Cipriani kulihamia Malindi, mji wa kitalii waliyoizuru tangu miaka ya 1980.
Waliamua wakiwa Kenya wataisaidia jamii ile haswa watoto ambao kila wakati wao ndio huhadhirika. Walianza kwa kuunda mradi wa kujimudu pale Makombeni plateau, ambao ni mtaa uliokumbwa na umasikini mkubwa.
Tangu mwanzo mradi ulijimudu kupitia ushirikiano baina ya Watoto Kenya Onlus na wakaazi wa jamii ile pamoja na miradi midogo midogo.
Watoto Kenya Onlus ilifadhili kifedha ujenzi wa jumba uliokuwa makaazi ya watoto 30, shukrani kwa uwepo wa ardhi uliotayarishwa na walimu wa wale watoto.
Lengo kuu la chama ni kusaidia watoto wasiyojiweza, waliotelekezwa,mayatima na wenye maradhi ya UKIMWI pamoja na vijana barubaru.

Kwa miaka iliyopita, Watoto Kenya Onlus iliweza kuwapa watoto elimu katika shule za uma na gredi ya kwanza, 1795680_316961498507109_9002690559785871707_ngredi ya pili na usaidizi wa chuo kikuu pia katika kazi, kwa wale watoto walioishii ndani ya jumba lao. Pia chama iliwasaidia kifedha watoto kutoka familia maskini ambao walikua na talanta mbalimbali.
Mwanzoni jumba lao iliashiria pahali palipofunguliwa kwa jamii ya pale na shughuli mbali mbali zilikuwepo kwa ajili yao.
Safari kadha wa kadha zilipangwa ilikuweza kuifahamu vyema mazingira na jamii walioingia. Pia walianzisha gazeti ndogo iliyosambazwa katika vijiji karibu nao. Walifungua zaanati na kuanza uhusiano wa kikazi na ofisi ya Malindi Child Protection Center.

Watoto Kenya Onlus wangependa kuifanya mradi iweze kujimudu na kuwezesha uchumi wa jamii kujistawisha. Lengo hili limekamilika kwa miezi mitatu pekee katika mwaka mzima – shukrani kwa ufugaji wa kuhama, uvuvi na maabara ya ushanaji nguo.
Ukuzaji na uuzaji wa vyakula, maziwa na mikoba pamoja na vyombo vingine inawahakikishia uchumi uliostawi na kuwezesha jamii kufanya kazi.

Watoto Kenya Onlus ingependa kufikisha jumba lile la watoto kiwango ambayo linaweza kujimudu ili kuwawezesha wafanyakazi wa kjitolea kutoka ndani ya jamii kuwa na elimu(ujuzi) na uwezo wa kuiga na kufanya vile vile katika sehemu zingine za Kenya.

Tuliwauliza kuhusu shughuli zao hapa Italia.
Kule Italia chama hufanya kazi na watu wa kujitolea kutoka upande nyingi za Italia; Roma, Padua, Arezzo, Bassano del Grappa, Milan, Turin, Genoa. Kuna mikakati mingi hata soko mashinani, ili kusanya hela na pia kujuza jamii mashinani.
Yeyote angependa kujitoa kufanya na chama hichi anaweza wasiliana nao kwa urahisi na kutoa maarifa na wakati wao. Safari ya ng’ambo hupangiliwa kwa vikundi vidogo ili kuweza kuelewa tamaduni ya jamii na kuishii nao wakati usio na kifani.

Walitacha na changamoto ilio na maana ya ndoto na vile ya kuifanya kweli: “ukiota pekee yako, ni ndoto tu, lakini tukiota pamoja ni ukweli inayoanza”.

Tunawashukuru Lara na Francesco na rafiki wote wa Watoto Kenya Onlus kwa urafiki na mapenzi yao.Tutaendelea kuwakumbatia watoto wa Kenya katika safari zetu!

10734253_317612901775302_46501596492183769_n

Traduzione a cura degli amici kenyoti di Maralal