browser icon
You are using an insecure version of your web browser. Please update your browser!
Using an outdated browser makes your computer unsafe. For a safer, faster, more enjoyable user experience, please update your browser today or try a newer browser.

Africa Milele Onlus

logo_onlus copia

Contact Person: Lilian Sora; Telephone Number: +39 3482421299; E-mail: info@africamilele.org;
Website: www.africamilele.org

Tulikutana xlestrade ya Turin, Lilian Sora pamoja na Luca Lombardi ambao ni Raisi na katibu wa chama cha Africa Milele Onlus pia ni bwana na bibi katika maisha.
2013-09-09 18.46.17Africa Milele ni chama iliyoanziswa kule Fano, mkoa wa Pesaro e Urbino, wa Marche region, tarehe 9 septemba 2012.
Wazo hili iliwajia baada ya fungate yao kule Kenya, mwaka wa 2009. Walipata fursa ya kuwafahamu watu na rafiki wapya ndipo wakaamua, baada ya mazungumzo kadha wa kadha, kuifanyia inchi ile jambo ambalo walihisi kujitoa kwa hali na mali.
Kama tujuavyo neno “milele” huusisha kujifunga katika jambo fulani hisia za undani.

Kabla ya kuifadhili chama, walifanya utafiti na kubuni mikakati itakayo waongoza, huku wakiwahusisha wazazi wake Lilian.

Lilian aliieleza Xlestrade ya kuwa mradi huu ulichaguliwa na kuafikiwa baada ya safari zingine kenya pamoja na mkutano na Salvatore Fabrizio, raisi wa chama cha Karibu Onlus katika jiji la Milan, ambaye kwanza alijuzwa kutumia e-mail kufuatiwa na mawasiliano.

Karibu Onlus hufanya kazi Kenya, Chakama ilioko 70km mbali na Malindi.
Miradi ya Africa Milele yana lenga hasa jamii ya chakama wakishirikiana na Karibu Onlus, ingawa inajitegemea. Lengo la chama nikuwezesha jamii hii kujitegemea.
Makao makuu ya chama yako Malindi, ambayo ni mji wa karibu na mombasa hivi kwamba inawezesha mawasiliano ya kimtandao na pia inawezesha wepesi wa kufika jamii ya chakama.

Lengo kuu ni kujenga makao ya watoto yatima itakayokuwa malazi ya watoto 24 (waliopoteza wazazi wote).watoto hawa watapokea huduma ya afya an fursa katika elimu kulingana na uwezo wa kielimu, asante kwa mradi wa “distance adoption project.”
Mfumo wa photovoltaic itakayo ondoa ukosefu wa nguvu za umeme umeandaliwa na hivi karibuni itatundikwa 2013-08-03 10.36.13kwenye mjengo. Watoto wataingia jumbani mwisho wa mwaka wa 2013, wa wafanyakazi wote ni wanajamii ya chakama. Lilian na Luca walitueleza kuwa jumba hili limebandikwa jina “Mvua Bahati”, kwa sababu walipoiona ardhi ile kwa mara ya kwanza ilinyesha mvua, ambayo ni ishara ya bahati katika utamaduni wa kiafrika.
Hivi sasa kule Kenya kuna mvulana kutoka Italia, Ivan Gidiuli. Ndiye meneja, mwelekezi wa shughli zote tangu mwisho wa Julai.

Xlestrade iliwauliza malengo yao ya siku za usoni:
Wakajibu kuwa wangependa wawehuru, walinunua vyombo na mbao ya kutengeneza tanuri ya mbao, shukrani ziwaeleke wafanyakazi wakujitolea (kutoka vyama vyote viwili.) walioenda kenya mwezi wa agosti 2013. Lile tanuri litakuwa raslimali ya muhimu sana katika siku za usoni kwa jamii na hatua muhimu ya kwanza kuafikia uhuru iliozungumziwa awali.

Kuna shughuli mbalimbali yalio pangwa hapa Italia ili kuweza kupata ufadhili wa kuendelesha mradi, kama vile; mashindano, sherehe na njia zinginezo zitakazo wawezesha kuwafikia wafadhili.chama pia ilianzisha uhusiano na makampuni na taasisi pia kufanya kazi na shule za Fano.

Xlestrade iliwauliza jinsi ya kushirikiana na chama yao; Lilian aliwaeleza kuwa wanaweza kuchangia kwa kujisajili kuwa wanachama na kulipa karo ya wanachama. Pili, wanaweza shirikiana katika uboreshaji wa shughuli za chama. Tatu, kuna wezekano wakufanya utarajali na vikundi vya wanaoishi Kenya na safari yanaweza pangiliwa wakati wowote wa mwaka.

Mwisho tuliwauliza kutuacha na sentesi moja ya kutafakari, Lilian na Luca walichagua sentensi ya Ivan kuhusu historia ya Africa Milele vizuri sana: “Chakama ni moyo inayoelezea kuhusu sababu”.

Xlestrade inawashukuru sana kuaajili ya mkutano huu na kuhusika kwao katika mradi wao.
Tulipata kujuana kupitia Facebook na tunadhamani sana fursa hii nakuendeleza uhusiano huu.
Muwe na safari njema Africa Milele!!!

cuore

Traduzione a cura degli amici kenyoti di Maralal